kijana wa bodaboda anusulika kuuwawa baada ya kuiba mkoba
Dah!
hii hatari sana. kijana mmoja wa bodaboda maeneo ya Sinza Afrikasana
jijini DSM ambaye jina halikupatikana, alikoswakoswa kuuawa baada ya
kupora mkoba uliokuwa na simu ya mwanamke aliyekuwa akipita njia. Cha
ajabu kijana huyo alivyokwapua mkoba, pikipiki iligoma kuwaka basi raia
wenye hasira kali wakaanza kumshushia kipigo kikali. Kijana aliponea
chupuchupu kuchomwa moto, kwani waliokuwa wamefuata mafuta ya petroli
waliporudi walimkuta trafiki akizuia asiuawe basi raia hao walihamishia
hasira zao kwenye kuichoma moto bodaboda ya kijana huyo.
Comments
Post a Comment