Yaya Toure Afikiria Kumfuata Kolo Toure
Kiungo Gnegneri Yaya Toure amesema anafikiria kustaafu soka ya kimataifa baada ya kutimiza malengo yake.
Toure aliiongoza nchi yake kama nahodha kutwaa ubingwa wa mataifa ya
Afrika, hilo likiwa taji la kwanza kubwa baada ya zaidi ya miongo miwili
na sasa anaweza kufuata nyayo za kaka yake, Kolo kuvua jezi Ivory
Coast.
Toure amesema atachukua siku kadhaa kuamua mustakabali wake, lakini
amependekeza, kizazi kipya sasa lazima kipewe nafasi kikosi cha tembo.
"Mustakabali wangu?' aliuliza, alipoulizwa na BBC.”Inabidi usubiri.
Sasa, malengo yangu yametimia. Tunapaswa kusubiri kwa siku kadhaa na
kuona tutafanya nini,".
"Kaka yangu amestaafu, na Copa (Barry, kipa wa muda mrefu wa Ivory
Coast) naye pia. Muda wa nyota wanaochipukia utafika karibuni.
Tunahitaji kuwaachia wao.
Maneno haya ya Toure yanaweza kuwa habari njema kwa klabu yake,
Manchseter City, ambayo ilikuwa katika wakati mgumu kwa kumkosa mchezaji
huyo alipokuwa kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Equatorial
Guinea.
Comments
Post a Comment